Wednesday, September 22, 2010

KUSANYIKO LA BWANA-KIBAHA PRECIOUS CENTRE

 SHALOM!! Jiandae na Kusanyiko la Bwana Litakalofanyika pale EFATHA H/Q KIBAHA PRECIOUS CENTRE...kuanzia tarehe 4/10/2010-10/10/2010 ni kusanyiko la kuvikwa silaha zote za MUNGU....wahubiri wa kimataifa kutoka nchi mbalimbali watakuwepo wakiongozwa na MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA,njoo uone matendo makuu ya MUNGU...Mass Choir wataongoza sifa na kuabudu!! karibu sana umualike na mwingine kwa maelezo zaidi tembelea katika vituo vya EFATHA vilivyopo DAR ES SALAAM na mikoani..na Nje Ya Nchi pia..Mungu akubariki sana!!

Nyumba Ya Makimbilio

 Efatha Ministry: ni huduma ya Ukombozi na Uponyaji iliyoanzishwa mnamo mwaka 1992 na kusajiliwa rasmi kisheria mwaka 1997...Mwanzilishi wake ni MTUME NA NABII JOSEPHAT ELIAS MWINGIRA aliyepokea maono haya akiwa huko MERERANI mkoani ARUSHA.Imekuwa ni huduma ya kipekee kwa wale waliokosa matumaini na mahali pa kutua mizigo iliyowaelemea katika maisha yao....yawezekana kabisa unao uhitaji wa uponyaji na ukombozi katika maisha unayopitia....tembelea LEO katika Kituo kikuu kilichopo Mwenge Dar Es Salaam...kina choongozwa na MTUME NA NABII au MAKAO MAKUU yaliyopo KIBAHA(PRECIOUS CENTRE)na vituo vingine mikoani na hata nchi za nje....ikiwa umewahi kusikia habari za EFATHA tafadhali changia hapa kueleza yale ambayo Mungu amekufanyia kupitia huduma hii ili na wengine wapate kuinuliwa na Ushuhuda wako.....Ahsanteni sana na Mungu awabariki sana!!